Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa timu yake kwa sasa haiwezi kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kufungwa 4-0 na Everton kwenye uwanja wa Goodson Park.

Manchester City wapo nyuma kwa alama 10 dhidi ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea wenye alama 52 mpaka sasa.

Kocha huyo amesema kuwa alama 10 ni nyingi sana na si rahisi kuzifika kwa haraka kutokana na viwango vya timu zilizopo juu yake.

Guardiola, mwenye miaka 45, amewaambia wachezaji wake kuungana wakati huu wa kipindi kigumu na kutoangalia msimamo wa ligi mpaka mwisho wa msimu.

Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa ana furaha sana kuwa ndani ya Manchester licha ya timu yake kuwa nafasi ya tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *