Kampuni ya GSM imemteua mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuwa Balozi wa bidhaa za kampuni hiyo hapa nchini.

Diamond Platnum amekuwa Balozi wa Bidhaa za GSM na kuwataka watanzania wanunue bidhaa hizo kuacha kutumia gharama kwa kufuata nje ya nchi.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa licha ya kuwa balozi katika bidhaa za GSM ameweza yeye kununua kutokana vitu mbalimbali katika maduka hayo.

Diamond amesema kuwa GSM walikuwa na uwezo wa kutafuta wasanii wa nje ya nchi lakini wakaona kuna umuhimu wa kuwatumia wasaani wa ndania kama mabalozi katika bidhaa zao.
mondi

Pia amesema kuwa ubalozi huo utafanya kutangaza muziki wake kwa mashabiki wa ndani na wan je ya nch.

Diamond amesema kuwa balozi hakuathiri ubalozi mwingine kutokana kuwa kinachotangazwa ni bidhaa ambazo haziingiliani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *