Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ameachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana hiyo kwa masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni tatu.

Lema amekaa mahabusu kwa takribani miezi minne sasa tangu alipokamatwa mwezi Novemba mjini Dodoma na kusafirishwa kupelekwa Arusha kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi.

Jaji Salma Magimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ndiye atakayesikiliza rufaa hiyo namba 126 ya mwaka jana ambayo iliwasilishwa na mawakili wanaomtetea, Kibatala, John Mallya na Sheck Mfinanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *