Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amewajia juu watu ambao wanatumia jina lake kujipatia fedha kiutapeli kupitia mitandao ya kijamii.

Gabo kuptia akaunti yake ya Instagram ameonesha kuchukizwa na kitendo hiko kutokana na baadhi ya watu kutumia jina lake kujipatia fedha kiutapeli.

Muigizaji huyo ameandika ‘Jamani watanzania mbona mnafanya hivii

??kwanini lakini Tunachafuana? Huu ni utapeli umekuwa ukiendelea kila mara na sasa umeshika kasi na nguvu.

Pia ameongeza kwa kuandika “Gabo hawa wasiokuwa mimi wamekuwa ni wengi mno huku wakiwatapeli watu kwa nafsi ya kuuza bidhaa mbalimbali au Kudhulum kwa mifano hii tafadhari tabia hii ikome.

Tabia hiyo ya baadhi ya watu kutumia majina ya mastaa nchini kutapeli watu imekuwa maarufu mjini kwenye mitandao ya kijamii kwasasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *