Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Crazy GK amesema viongozi wengi wa Afrika kwasasa hawana uzalendo wala utu wametanguliza maslahi yao mbele kiasi cha kutojali wananchi na kupelekea kuwaua watu wasio na hatia.

GK amesema viongozi wengi wa Afrika wapo tayari kuona watu wanakufa ili wao waendelee kubaki madarakani na kuendelea kuongoza nchi ili hali labda hata wananchi hawawataki.

Vile vile mkali huyo aliyewahi kutamba na wimbo ‘Hii Leo’ amesema viongozi wa sasa wa Afrika ni wauaji wapo tayari kuona watu wanakufa ili wao waendelee kubaki madarakani.

Kwa upande mwingine GK amewatolea mfano viognozi kama vile Mwalimu Nyerere na Mandela wawe mfano wa kuigwa kwasababu walikuwa wapo tayari kufa kwa ajili ya kuwalinda na kuwapigania wananchi wao.

Rapa huyo mkongwe pia amesema viongozi wa saizi wanang’ang’ania madaraka wanatumia nguvu za dola kuwadhuru watu ili wao waendelee kubaki madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *