Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, King Crazy GK amefunguka na kusema kuwa kwasasa hataki tena kufanya show ambazo hatalipwa fedha chini ya milioni 30.

Crazy Gk ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mzuri Pesa’ aliyoifanya kwa kuimba amesema kuwa kwasasa mtu yeyote anayetaka kufanya naye kazi lazima awe amejikamilisha ndiyo afanye tena kazi.

Crazy Gk amesema “Kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi lazima awe amejikamilisha kwa sasabu ukiangalia wasanii wanaotoka nje ya Tanzania wakija huku wanalipwa hadi milioni 100 lakini sisi wa ndani hela inakuwa ndogo naamini tunaweza na muziki tunaofanya ni mzuri media zikiendelea kusapoti naamini hata sisi tuna uwezo wa kulipwa hela hizo’

Mkali huyo aliyetamba na nyimbo zake za kitambo kama vile Sister sister, Hii Leo, Ama zangu ama zao, Sauti ya Manka pamoja na Ntakufaje amesema kwasasa amepanda bei kwa hiyo lazima wadau wajipange kama wanataka kufanya nae kazi.

Kiongozi huyo wa East Coast Team alikuwa anaimba hip hop kwasasa amebadilika na  kuamua kuingia kwenye Bongo flava.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *