Kiongozi wa zamani wa kundi la East Coast team, Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy GK ambaye aliwahi kujitamba kuwa HIP HOP anayoifanya yeye haiwezi kufikiwa na wasanii kutoka upande mwingine wowote Tanzania, amegeukia kuimba.

Staa huyo aliyejenga jina na heshima kupitia ngoma za HII LEO, NITAKUFAJE na SAUTI YA MANKA amekiri kuwa badiliko kubwa la upepo wa muziki wa Bongo Fleva umemfanya kugeukia ‘KUIMBA’ na kuachana na ‘KURAP’.

GK ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu sana ameyasema hao wakati anatangaza ujio wake mpya kwenye Bongo Fleva huku akiwataka mashabiki wake wajiandae kuona ‘versatility’ yake.

Kundi la East Coast ambalo lilimtambulisha kama ‘Kamanda na Amiri Jeshi Mkuu’ lilikuwa likiundwa na mastaa kibao wakiwemo AY na Mwana FA ambao hata hivyo baadae walijitoa baada ya kupishana na GK.

Hata hivyo mastaa hao watatu wamemaliza tofauti zao na wako tayari kusaidiana kwenye kazi zao.

Soko la muziki wa kuimba kwenye Bongo Fleva kwa sasa limetawaliwa na mastaa kadhaa wakiwemo Ali Kiba, Diamond Platnumz, Ben Pol n.k

Huku rapa na kiongozi wa Tip Top Connection, Madee akiwa na nyimbo moja inayokosoa soko la muziki wa Hip Hop hapa Bongo.

GK ataweza kuwashawishi mashabiki waachane na Ali Kiba, Diamond Platnumz, Ben Pol na wengineo na wamsikilize yeye?

GK ameahidi kuachia ngoma za mahadhi mbalimbali kwenye ujio wake mpya huku mashabiki wakisubiri zaidi iwapo atatoa nimbi ya taarabu kwakuwa muziki huo hauna mfalme tena.

GK kuja na ngoma ya taarabu ‘tusubiri tuone ujio mpya wa Kamanda’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *