Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, King Crazy GK amewataka mashabiki wa muziki huo kuendelea kusubiria kazi mpya za kundi la East Coast Team ambapo wapo kwenye maandalizi ya kazi mpya.

GK amesema kundi hilo litarudi kama zamani na kutoa nyimbo mpya kwaajili ya kurudisha heshima ya kundi hilo ambapo kwasasa heshima hiyo imepotea baada ya kukaa kimya katika ramani ya muziki.

Staa huyo huyo ambaye ameachia video ya wimbo mpya ‘Mzuri Pesa’ hivi karibuni, amewatoa hofu baadhi ya mashabiki ambao walikuwa wanasubiria kwa hamu project mpya za kundi hilo.

Mkali huyo wa ‘Ntakufaje’ ameongeza kwa kusema kuwa hakuna tatizo kati yake pamoja na AY na FA kwahiyo wanaweka sawa mpango wa kurudi kwa kundi hilo kutoka maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam.

Pia Gk amewataka mashabiki wasiwe na wasiwasi kila kitu kipo sawa kabisa kwasaababu kuna nyimbo mbili na zote zinafanyiwa maandalizi ya video kwahiyo mambo makubwa yanakuja ndani ya kundi hilo.

Pia rapper huyo amesema wameajiri watu wa masoko kwa ajili ya kuibrand East Coast pamoja na yeye ili kuupeleka muziki katika level nyingine.

East Coast Team: Baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo.
East Coast Team: Baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo.

East Coast Team ni miongoni mwa makundi ya  muziki yaliyojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kutokana na vibao vyao kubamba masikioni mwa mashabiki wao kama vile ‘Hii Leo’, ‘Hama zangu hama zao’, Itikadi na nyingine kibao.

Wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo ni GK, AY, FA, Snair, Buff G, Pauline Zongo, Stany Boy pamoja na Sharifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *