Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, King Crazy GK amefunguka na kutoa ushauri kwa msanii Diamond Platnumz na kumtaka kuwa na kitu kingine kwa sasa nje ya muziki kwa kuwa muziki una kawaida ya kupanda na kushuka.

GK amesema hiyo itamsaidia endapo ikitokea muziki umeshuka upande wake, aendelee kunufaika na kuingiza pesa kwa miradi mingine ambayo inamfanya azidi kuwa juu siku zote katika maisha.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz

King Crazy GK amesema biashara ya muziki ina kupanda na kushuka hivyo kwa jina alilonalo saizi Diamond Platnumz anapaswa kulitumia kufanya biashara nyingine nje ya muziki ambayo inaweza kumuingizia pesa zaidi ili hata siku muziki ukibadilika maisha yake yaendelee kubaki juu.

GK ni mwanamuziki mkongwe aliyetamba miaka ya nyuma akiwa na kundi la Eat Coat Team ambapo alitamba na nyimbo kama vile ‘Sister sister’, ‘Ntakufanye’ Sauti ya Manka pamoja n Hii Leo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *