Mastaa wa Marekani, Ginuwine, Mya na kundi la 112, wanatarajia kutumbuiza katika tamasha la The Plot litakalofanyika katika ukumbi wa Ngong Racecource Waterfront jijini Nairobi nchini Kenya ifikapo Agosti 13 mwaka huu.

Ginuwine alikuwa msanii wa label ya Epic Records katika miaka ya 1990 na amewahi kutoa albamu na single zilizouza platinums na kuwa mmoja wa wasanii waliowika sana mwishoni mwa 1990.

Mya
Mya

Mya ni msanii aliyesaini na Interscope Records mwaka 1998 na kuachia albamu yake mwaka huo huo iliyofanya vizuri sokoni nchini Marekani ikiwa na single ‘It’s All About Me’.

112 ni kundi la vijana wanne lililokuwa chini ya label ya P. Diddy, Bad Boy Records na Def Soul na Wamewahi kutoa ngoma zilizofanya vizuri kama “Only You”.

112
112

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *