Video vixen Bongo, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa anatamani kutoka kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Gigy Money aliweka picha akiwa na Diamond katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha akiwa na Diamond Platnumz katika pozi tofauti.

Kilichozua gumzo zaidi katika posts hizo ni caption za Gigy Money zilizo onyesha dhahiri kuwa mrembo huyo anamzimikia Diamond Platnumz.

Akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha Radio maarufu nchini Gigy Money amethibitisha ni kweli anamtamani kutoka kimapenzi na Diamond na wala hajali kama yeye ana familia.

Katika mahojiano hayo Gigy Money amesema kuwa Diamond Platnumz amekwisha onyesha utayari wa kutoka naye kimapenzi ila mambo mengine yanatakiwa kubaki kuwa siri yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *