Video Vixen wa Bongo, Gigy Money ameendelea kuzikamata headline wiki hii baada ya kumtaja mkali wa Bongo fleva Alikiba kuwa ndiyo mwanaume aliyekuwa anamuonga sana kuliko wanaume wake wote.

Gigy Money amesema kuwa kati ya wanaume wake wote hawezi kumsahau Alikiba kwasababu alikuwa anamhonda vizuri kuliko wanaume wake wengine.

KIBA

Video queen huyo amesema kuwa aliweza kusoma kutokana na pesa ambazo alikuwa anahongwa na muimbaji huyo.

Kwa upande mwingine Gigy Money amesema kuwa anahisi Alikiba hajataka awe video queen kwenye video zake kutokana na kuwa naye kwenye mahusiano katika kipindi cha nyuma ambapo kwasasa hawapo kwenye mahusiano.

Video queen huyo kipindi cha nyuma aliwahi kuwataja wanaume wake aliowahi kutembea nao ambao ni wasanii wa Bongo fleva akiwemo Abdukiba ambaye ni mdogo wake Alikba pamoja Rich Mavoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *