Video queen maarufu Bongo, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nampa papa’ ni bora kuliko ‘Seduce Me’ wa Alikiba.

Gigy Money amesema kuwa kwa maoni yake na watu wengi anaona Nampa papa ni kali sana kuliko Seduce me ya Ali Kiba.

“Ni hivi Seduce me na ngoma yangu nampa papa yangu kali, ndiyo Nampa papa kali kuliko seduce me yaani itakaa muda mrefu kwenye chati sema tu watu hawataki kukubali hili.

Pia amesema kuwa mashabiki waliupokea wimbo wa Aliba kwa sababu Alikiba ni msanii mkubwa alafu alikaa kimya muda mrefu mashabiki walimmiss sana alafu huwezi kusikiliza seduce me zaidi ya mara tano lakini papa unaweza kusikiliza kila siku.

Alikiba ambaye kwa sasa bado anafanya vizuri na wimbo wake wa Seduce me alioutoa mwezi uliopita amekuwa akipata maoni mbalimbali juu ya wimbo huo kutoka kwa wasanii mbalimbali mmoja wapo akiwemo Gigy Money.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *