Video queen Bongo, Gigy Money amefunguka sababu zilizkuwa zinamfanya apige picha za utupu licha ya kitendo si kizuri kwa jamii.

Gigy Money amesema kuwa sababu iliyomfanya apige picha za utupu ni kwa ajili ya kupata pesa ambazo anapeleka nyumbani kwao, licha ya kitendo hicho kutokuwa kizuri kwa jamii.

Gigy Money ambaye kwasasa amejikita kwenye masuala ya kuimba amesema kuwa wazazi wake waliridhia kitendo hicho kwani pesa ambayo alikuwa anapata zinaenda nyumbani.

Pia amesema kuwa picha hizo alikuwa anapiga kwa ajili ya kufanya tangazo la nguo za ndani na sio vinginevyo.

Gigy amesema kuwa “Mimi mama yangu, wazazi wangu na ndugu zangu fresh tu kwao kwa sababu nilikuwa napeleka hela nyumbani, sio kama nilikuwa nafanya vile bure, au nilikuwa namtangazia mtu makalio yangu hapana, nilikuwa nalipwa kutangaza brand ya nguo za ndani, ilikuwa ni rahisi kufanya kwa sababu nilikuwa napata hela”,.

Gigy Money ambaye kwa sasa amepunguza mwili wake alipata umaarufu kwa kupiga picha za utupu ambazo zilileta gumzo kwa jamii, mpaka sasa ameamua kuingia kwenye muziki ili kujipatia kipato kwa shughuli ya halali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *