Kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ameteuliwa kuwa kocha mpya klabu ya Rangers ya nchini Scotlannd kwa mkataba wa miaka minne.

 

Gerrard mwenye umri wa miaka 37 anachukua nafasi ya Graeme Murty aliyekuwa  kocha wa muda wa klabu ya Rangers kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Pedro Caixinha mwezi Oktoba mwaka jana.

 

‘’Nimefurahi kuteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Rangers, ninaiheshimu klabu hii na historia yake’’,.

 

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza alicheza michezo 710 na kufanikiwa kushinda jumla ya vikombe 9 akiwa na klabu hiyo.

 

Changamoto mpya anayokwenda kukutana nayo Gerrard ni kwenda kupambana na aliyekuwa kocha wake wakati akicheza Liverpool Brendan Rodgers ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Celtic, mabingwa wa ligi kuu ya Scotland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *