Nahodha wa zamani wa Liverpool na Uingreza, Steven Gerrard amechaguliwa kuwa kocha wa timu ya vijana ya Liverpool baada ya kustaafu soka.

Gerrard mwenye miaka 36 alianza kuchezea Liverpool mwaka 1998 anatarajia kuanza kazi yake ya ukocha katika kikosi cha vijana ifikapo Februari mwaka huu.

Kiungo huyo aliondoka kwenye klabu ya Liverpool mwisho wa msimu wa 2014-15 na kujiunga na klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani na kustaafu soka Novemba mwaka jana baada ya kucheza mpira kwa kipindi cha miaka 19.

Baada ya kustaafu soka kiungo huyo alihusishwa na kujiunga na klabu ya MK Dons inayoshiriki ligi daraja la kwanza ili awe kocha lakini hakuvutiwa na ofa hiyo.

Gerrard amecheza mechi 710 akiwa Liverpool ameshinda mataji tisa pia amecheza mechi 114 timu ya taifa ya Uingereza na kukiongoza kikosi hiko kwa kipindi cha miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *