Hatimaye maziko ya aliyekuwa staa wa Pop, George Michael yamefanyika ikiwa ni miezi mitatu tangu alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 53.

Familia ya staa huyo ilisema kuwa ‘shughuli ndogo na binafsi ya mazishi’ ilifanyika siku ya jana na waliohudhuria ni wanafamilia na watu wa karibu.

Kwenye taarifa yao, waliwashukuru wote wakiwemo mashabiki kwa ujumbe wao wa mapenzi na kuwaunga mkono kufuatia maziko hayo yanayodhaniwa kufanyika kwenye jiji la London.

Kifo cha staa huyo aliyefariki siku ya tarehe 25 Disemba mwaka jana kimethibitishwa kusababishwa na sababu za kawaida na hakukuwepo na dalili zozote za njama za kumuua au matumizi yaliyopitiliza ya vileo.

Taarifa kamili ya familia ya Michael kutokana na mazishi hayo inasema: ‘Tunapenda kuthibitisha kuwa mazishi ya muimbaji George Michael yamefanyika leo. Familia na marafiki wa karibu walikusanyika kwenye shughuli ndogo kuuaga mwili wa mpendwa wao, kijana wao na rafiki yao’

‘Familia ya George inapenda kuwashukuru mashabiki wake duniani kote kwa ujumbe wao wa mapenzi na faraja. Tunapenda ombi la familia la kufanya mambo yake binafsi liheshimiwe ili wanafamilia waweze kuishi maisha waliyozoea bila kubugudhiwa na vyombo vya habari’

Jina kamili ya George Michael ni Georgios Kyriacos Panayiotou na alianza kuvuma kwenye muziki kwenye miaka ya 1980 kwenye kundi la Wham! Akiwa na mwenzake Andrew Ridgeley.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *