Mkimbiaji wa Ethiopia, Genzebe Dibaba amevunja rekodi ya dunia yam bio za mita 2,000 kwa wanawake baada ya kushinda kwenye mashindano ya mbio za ndani ya Miting International de Catalunya.

Mkimbiaji huyo aliyetumia 5:23.75 ameivunja rekodi iliyowekwa mwaka 1998 na mkimbiaji wa Romania Gabriela kwa tofauti ya sekunde saba.

Mkimbiaji huyo mwenya miaka 25 sasa anashikilia rekodi ya dunia kwa mbio za ndani kwa mbio za mita 1,500m, maili moja, 2,000m, 3,000m, maili 2 na 5,000m.

Pia kwenye mbio za nje anashikilia rekodi kwenye mbio za mita 1,500m.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *