Gazeti la Raia Mwema ambalo ni gazeti la kila wiki, limefungiwa na serikali kwa siku 90 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo.

Idara hiyo imeeleza sababu za kusitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti hilo kuwa ni kutokana na kuchapishwa kwa toleo la tarehe 27 mwezi Septemba hadi 3 Oktoba 2017, lenye kichwa cha habari inayosomeka, “URAIS UTAMSHINDA JOHN MAGUFULI.”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imesema kuwa gazeti hilo limetoa nukuu zisizo za ukweli kuhusu Rais John Magufuli, japo imekubali kuwa ni haki ya gazeti hilo kutoa maoni.

Hili ni gazeti la tatu kufungiwa ndani ya miezi minne, ikiwemo gazeti la MwanaHalisi lilifungiwa wiki iliyopita kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchapishaji wa habari za uongo na kuchochea ambazo inadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *