Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amekabidhi jumla ya shilingi milioni 23 kwa familia tatu za manusura wa ajali ya watoto wa Lucky Vicent.

Gambo amesema fedha hizo zilikuwa Zimebaki baada ya matumizi ya shughuli za mazishi kwa watoto 32 walimu wawili na dereva.

Wazazi wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada mkubwa kwa watoto wao tangu mwanzo hadi sasa.

Kwa mujibu wa Gambo, baada ya kutokea kwa ajali hiyo mwezi Mei 2017, wadau mbalimbali na serikali walijitolea na kuchanga fedha na kupatikana zaidi ya milioni 285.49 ambazo nbaada ya matumizi zilibaki milioni 23.27 ambazo zilikabidhiwa jana

Pia Gambo alisema Serikali imekubali kutoa wataalam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto hao ili kuwaweka sawa na kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la 7 unaowakabili mnamo mwezi Septemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *