Mwenjeji wa kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) Gabon imeaga mashindano hayo kwenye hatua ya makundi baada ya jana kutoka 0-0 dhidi ya Cameroon katika raundi ya tatu ya michuano hiyo.

Gabon imeambualia alama tatu katika mechi zake zote tatu baada ya kutoka sare mechi zote bila kupata ushindi wa hata mechi moja hali ambayo iliyosababisha kuondoka mapema katika hatua ya makundi.

Timu hiyo iliyokuwa kwenye kundi A pamoja na timu za Burkina Faso, Cameroon na Guinea imemaliza nafasi ya tatu akiwa na alama 3 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Burkina Faso mwenye alama 5 pamoja na Cameroon mwenye alama tatu pia, nafasi ya mwisho ikishikwa na Guinea mwenye alama 1.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo Burikina Faso wameitandika Guienea goli 2-0 na kufanikiwa kuongoza kundi A kwa tofauti ya magoli na Cameroon ambao wote wana alama tano kila mmoja.

Mechi za michuano hiyo zinaendelea tena leo kwa kundi B katika viwanja viwali tofauti Senegal itacheza dhidi ya Argelia na Tunisia itacheza dhidi ya Zimbabwe.

Senegal tayari imeshafuzi hatua ya robo fainali baada ya kushinda mechi zake mbili za hapo awali na kujikusanyia alama sita na goli 4.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *