Staa wa Bongo movie, Gabo Zigamba amesema wasanii wa movie wanapaswa wasome ili kufanya kazi zenye uhakika zaidi na kuwaletea kipato.

Gabo ameyasema hayo wakati akimuongelea muigizaji, Rachel Bithulo ambaye ni msomi mwenye Shahada ya Biashara ambapo ameigiza kwenye filamu yake mpya na kusema anajua anachokifanya.

Staa huyo amesema kwamba tasnia ya filamu inaonekana inakufa kwa sababu ya kukosa watu makini, lakini endapo wasomi kama Rachel watajitokeza, wataifanya sanaa ikue na kurejesha heshima inayoonekana kupotea.

eee

Gabo amesema kwamba Rachel ni msanii mzuri, anamtabiria kuja kusumbua sana mbele ya safari yake ya uigizaji pamoja na kuleta changamoto katika tasnia ya filamu kutokana na elimu yake aliyoipata.

Muigizaji huyo amesema kitu kinachomfurahisha kwa Rachel ni kuwa tofauti na waigizaji wengi wa kike, kutokana na kuwa msomi na ana elimu kubwa, kwa hiyo wakiwapata watu kama hao watasaidia kuirudisha tasnia kama ilivyokuwa hapo awali kwa sababu hawaji kwa malengo yao bali kuokoa sanaa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *