Mastaa wa Bongo movie, Gabo Zegamba, Shamsa Ford na Irene Paul wanatarajia kuigiza pamoja katika filamu mpya ijayo inayokwenda kwa jina la ‘Karibu Kiumeni’.

Mtayarishaji mkongwe wa filamu nchini, Daniel Manege ambaye ameandaa filamu nyingi kama Dereva Taxi, Bado Natafuta, Nakwenda kwa Mwanangu pamoja na DJ Ben ndiye atayekuwa director wa filamu hiyo.

Matayarishaji huyo kupitia ukarasa wake wa instagram ameandika “Miamba miwili Daniel Manege wa safari ya Gwalu na Going Bongo, wanakutana kutayarisha project ya kukata na shoka ya ‘Karibu Kiumeni’ itakayosheheni mafundi kuanzia kwenye production hadi waigazaji”.

Daniel Manege pia aliandika “Utakutana na Ernest Napoleon, Irene Paul, Shamsa Ford pamoja na Gabo Zigamba”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *