Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Gabo Zigamba ameufungukia mtandao mmoja wa nchini Kenya baada ya mtandao huo kuandika kuwa muigizaji huyo ni raia wa Kenya.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Gabo ameandika jinsi nchi hiyo ya Kenya inavyojimilikisha vitu vya Tanzania kuwa ni vitu vyao akitolea mfano mlima Kilimanjaro pamoja na Olduvai Gorge.

Pia muigizaji hayo ameitaka Serikali kuingilia masuala hayo kutokana na nchi ya Kenya kuendelea na tabia ya kujimilikisha vitu vya Tanzania.

 Kupitia akaunti yake Gabo ameandika

Kinachoweza kuondoa makucha haya ya majirani ni film tuu. Film is the best method of propaganda spreading. Na ili tufikie hapo ni kufanya kazi zenye ubora wa kidunia ili ziende duniani kufikisha ujumbe.. bado tuna deni kubwa la kuwavua nguo hawa wadhalimu.. hii vita ya nyenyenye za jirani viongozi wengi wana nafasi ya kuishiriki ila sioni ushirika wao. Nna hofu hata tukianza kutengeneza films za kuuambia ulimwengu juu ya machache yanayotangazwa na majirani mmh zisijeishia studio kisa ujirani mwema.. hio ni hofu yangu tuu.. kama trump anamuongelea Puttin on media vipi viongozi wa serikali yetu hawayaoni haya yote..? Mimi naamini serikali yetu inauwezo wa kuita press na media house za dunia na kuorodhesha yote yaliyodaiwa na wakenya kuwa yao na kuipa ujumbe serikali ya kenya . Mfano.. Tunajua mengi yatadaiwa kuwa ni raia tu binafsi na taasisi ndio zinajitamkia haya mambo. Yaani si kenyan government.
Lakini mimi najiuliz raia anapoongelea vitu kama Olduvai gorge ipo kenya mimi najiuliza darasani somo la historia kenya wanafundisha nini?
bado najiuliza wakenya wanafundishwa georaphia ya wapi mpaka waseme kilimanjaro iko kwao?
Mrisho mpoto miaka michache ilopita huko ughaibuni alishikishwa bendera ya kenya na wakenya,akaishusha bendera stegini. Hongera kwako mjomba. Sikupoteza nguvu zangu wakati wa kutoa mchango wangu kwako mjomba.. Ukitaka kuusimamisha moto nenda kwenye chanzo.. haya mambo ni ya history na geographia yaani namaanisha hutokana na elimu wanayopewa.. sasa swali ni kwamba kama oldivai na kilimanjaro ni viko kwao unashangaa nn wakisema Gabo ni wao au mpaka waseme Arusha nayo ni ya kwao

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *