Muigizaji nyota wa Bongo movie, Gabo Zigamba amesema kuwa hana tofauti na wasanii wenzake kama katika tasnia hiyo kama ambavyo imekuwa ikilalamikiwa na wengi.

Gabo amesema kinachomfanya aonekane ana tofauti na wasanii wenzake ni utoafuti wa mtindo wa maisha alionao lakini hana tatizo nao na anawapenda kwa dhati.

Gabo aliendelea kusema kwamba tofauti kubwa iliyopo kwake na wasanii wenzake ni matarajio yake ya kufanya utofauti kwenye tasnia ya filamu hapa nchini.

Muigizaji huyo alifanikiwa kushinda tuzo ya msanii bora wa kiume kwenye tuzo za EATV zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Disemba 10 mwaka huu.

Kwa upande mwingine muigizaji huyo anamilikiwa na kampuni ya muziki ya Vitamin Music Group Limited inayomilikiwa na msanii wa Bongo felva, Belle 9 baada ya kutambulisha kwenye uzinduzi wa nyimbo mpya ya mwanamuziki huyo ‘Give It To Me’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *