Mkali wa Bongo movie, Gabo Zigamba amesema sanaa ya sasa siyo kama ya zamani na kuna utofauti mkubwa kati ya zama hizo mbili kutokana na uigizaji.

Gabo Zigamba amesema sanaa ya sasa ina ujanja ujanja mwingi ingawa inalipa tofauti na ya zamani kutokana na watu wanaigizaji vitu vilivyopo katika jamii tofauti na sasa wengi uigiza maisha siyo halisi.

Muigizaji huyo amesema sanaa ya zamani ilikuwa ya ukweli lakini haikuwa na maslahi sana kulinganisha na sasa imekuwa kama ya ujanja ujanja lakini ina maslahi kutokana sasa hivi wanaingiza pesa nyingi tofauti na zamani.

Pia Gabo amesema pamoja na umaarufu alionao hajajutia kuwa maarufu kwani ameweza kutumia fursa hiyo kujitengenezea pesa zaidi tofauti na baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakisema wanajuta kupata umaarufu kwani unawanyima uhuru wa kufanya baadhi ya mambo.

Gabo amejipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza kwenye lafudhi ya Kimakonde kwenye filamu tofauti alizowahi kuigiza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *