Mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi duniani maarufu kwa jina la G7 yametofautiana na Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu makubaliano ya Paris.

Makubaliano hayo ni ya mabadiliko ya Tabia ya nchi ambayo yamelenga kupunguza hewa chafu duniani.

Viongozi wa G7 wametoa msimamo wao kuhusu Marekani kuwa endapo Trump hatokubaliana na makubaliano hayo basi Marekani itakuwa imejiondoa katika umoja huo wa G7.

Katika taarifa iliyotolewa na umoja huo imesema kuwa Marekani haitaungana na mataifa hayo yenye nguvu duniani katika makubaliano ya mabadiliko ya Tabia nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *