Mwanamuziki wa hip hop nchini, G Nako amekanusha tetesi kuwa wimbo wake mpya ’Go Low’ aliofanya na Jux amekopi kutoka mwanamjuziki, Flowking Stone wa nchini Ghana.

G Nako anawakilisha kundi la Weusi amesema kuwa inawezekana idea zikawa zimefanana lakini hakukopi wimbo huo.

Tuhuma hizo zimekuja pindi msanii huyo alipoiachia ngoma hiyo ndipo wadau na wapenzi wake kusema kazi hiyo imefanana  kuanzia jina mpaka ‘mixer’ za mdundo wa muziki huo ambao unafananishwa na ‘Go Low’ ya Flowking.

Aidha msanii huyo amesema haiwezekani mtu akawa ana-copy na ku-paste halafu akapata njia yake anayoitaka kama utakuwa na ‘vision’ katika kazi zako na kitu chako.

Vile vile G Nako amesisitiza kuwa laiti angejua au kusikia wimbo huo upo katika mzunguko asingeweza kupoteza muda wake kutengeneza video na kurekodi sauti.

Kwa upande mwingine amesema ‘idea’ kama hizo za aina ya Club huwa zinatokea akiwa studio na siyo kwamba anakuwa amejipanga kuzipania kuzifanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *