Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayewakilisha kundi la Weusi, G Nako amefunguka na kusema kuwa mapokezi ya Cover ya ‘Seduce Me’ wa Alikiba yamekuwa makubwa kuliko matarjio yake.

G Nako ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Energy’ amesema kuwa mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa sana kuliko alivyodhani wakati wa matayarisho ya ngoma hiyo.

Kwa upande mwingine G Nako amesema kuwa hapendi kuhusishwa na mambo ya u-team kwani yeye ni mwanamuziki na kila mwanamuziki anauwezo wa kufanya nae kazi mbali na team zao.

G Nako ameendelea kwa kusema kuwa mashabiki wanatakiwa kupenda muziki mzuri na siyo masuala ya u-team kwasababu suala hilo linarudisha muziki nyuma.

 G Nako anaungana na producer Man Water na wasanii wengine mbali mbali ambao wamefanya cover ya ngoma hiyo ‘Seduce Me’ wa Alikiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *