Mwanamuziki wa Hip-Hop nchini kutoka kundi la Weusi, George Mdemu maarufu kama ‘G Nako’ amefunguka kwa kusema kwamba watu wanaosema wasanii wa kundi hilo wanafunikana kwa kutoa nyimbo mfululizo hawana ufahamu mzuri kuhusu biashara ya muziki.

G Nako amesema kwamba wanachofanya Weusi ni kila msanii kusimama yeye kama yeye ambapo wanapotoa ngoma kwa kufuatana ni mbinu za kampuni kuliteka soko muda wote na si vinginevyo.

Weusi-1

Staa huyo ameongeza kwa kusema kwamba nyimbo zao muda wote ni kali ni vigumu kufunikana anapotoa Joh, akitoa yeye au Nikki jambo hilo linafanya sokoni waenee wao wenyewe.

Vile vile G Nako amesisitiza kwa kusema kwamba huwezi kukwepa kuisikiliza Alosto, Perfect Combo au wimbo wa Nikki ‘Sweet Mangi’ kwa hiyo watu waelewe tu hizo ni  mbinu za kibiashara zilivyo kuhakikisha soko linakuwa lao.

Kundi hilo la Weusi linaundwa na wasanii watatu wanofanya vizuri katika soko la muziki nchini na kimataifa ambao ni Joh Makini, G Nako na Nikki wa Pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *