Mwanamuziki wa hip hop wa Marekani, Future amesema kuwa Hip Hop inayofanywa na wasanii wa Afrika ni nzuri kwani inawavutia wasanii wengi wakubwa wa Marekani.

Future amesema hayo baada ya kumaliza show yake iliyofanyika siku ya jumamosi katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Future amesema Hip Hop ya Afrika inaelezea uhalisia wa Mazingira na ina’sound nzuri pia hata midundo yake inavutia kuisikiliza kwenye nyimbo zao.

Amesema kuwa “Hip Hop ya Afrika inasound vizuri sana inavutia kuisikiliza kwani imejaa ubunifu na huwa naingia studio kusikiliza midundo yake kuona kama ninaweza kufanya kitu“.

Mkali huyo amethibitisha kuwa tayari amefanya kolabo na mwanamuziki kutokan Nigeri WizKid.

Katika show hiyo msanii kutoka Afrika Kusini, Casper Nyovest alitoa burudani ya kufa mtu kwenye onesho hilo lililofanyika Leaders.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *