Viongozi wa mashtaka nchini Uswizi wameanzisha uchunguzi wa uhalifu kuhusu mchezaji wa zamani nchini Ujerumani, Franz Backenbauer na wengine watatu kuhusu ombi la Ujerumani la kombe la dunia la mwaka 2006.

Kama wanachama wa kamati andalizi ya kombe hilo wanatuhumiwa kufanya udanganyifu ,ulanguzi wa fedha na utumiaji mbaya wa fedha.

Baadhi ya uhalifu huo ulitekelezwa katika taifa la Uswizi lakini Backenbauer ambaye aliongoza ombi hilo amekana kuhusika na ufisadi.

Backenbauer amesema kuwa alifanya makosa katika shughuli yote ya ombi hilo mwaka 2000 lakini akakana kwamba kura zilinunuliwa.

Shirikisho la soka duniani Fifa lilianza kuwachunguza watu sita kwa jukumu lao katika ushindi wa kuandaa haki za kombe hilo la dunia mwaka 2006.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *