Mwanamasumbwi nyota wa Tanzania, Francis Cheka anatarajiwa kupanda ulingoni dhidi ya Vijender Singh kwenye pambano la WBO Asia Desemba 17 mwaka huu nchini India.

Cheka alitangaza kuachana na mchezo huo baada ya kutokea sintofahamu baina yake na wasimamizi wake.

Cheka amesema kuna baadhi ya mambo yaliyomkwaza hadi akatamka maneno ya kustaafu lakini anaamini ipo siku ataacha kucheza mchezo huo na kuendelea kuibua mabondia vijana.

Bondia huyo amesema kuna vyama na baadhi ya watu hukatisha tamaa kwa kushindwa kuonesha ushirikiano.

Cheka anatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa kuelekea India tayari kwa pambano hilo la kimataifa.

Cheka amesema ananolewa na Kocha wake Abdallah Abdul hivyo lazima amchape mpinzani wake huyo mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *