Bondia Francis Cheka amepigwa kwa Knockout (KO) ya raundi ya tatu na mpinzani wake Vijender Singh mjini New Delhi nchini India.

Baada ya mpambano huo Singh alijigamba kwa kusema Cheka aliongea sana kabla ya pambano lakini yeye aliamini juu ya uzito wa ngumi zake na amefanikiwa kuzitumia vyema kumnyamazisha mbongo huyo.

 

Cheka atapanda tena ulingoni Desemba 25 mwaka huu kuzipiga na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

 

Kabla ya kupigwa na Singh, mara ya mwisho Cheka alipanda ulingoni Februari 27 mwaka huu alimpomshinda kwa ponti Geard Ajetovic wa Serbia viwanja vya Leaders Kinodoni, Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *