Klabu ya Swansea City wamemfukuza kocha wao Francesco Guidolin kutoakana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo toka kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza.

Swansea aijashinda hata mechi moja toka kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu nchini Uingereza huku ikishika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi kuu.

Kocha wa zamani wa Marekani, Bob Bradley anatarajiwa kuachana na klabu ya Le Havre inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ufaransa ili kuchukua nafasi ya Guidolini kwenye klabu hiyo.

Wamiliki wa Swansea City, Steve Kaplan na Jason Levien pamoja na mwenyekiti Huw Jenkins walifanya mazungumzo na baadhi ya makocha akiwemo Ryan Giggs ili kurithi nafasi hiyo iliyoachwa wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *