Kampuni kubwa ya utengenezaji magari ya Marekani ya Ford imetangaza kupata faida kubwa kwa mwaka wa fedha uliopita inayofikia $10.4bn (TZS25tn) ambazo sehemu yake itagawiwa kama nyongeza ya malipo kwa wafanyakazi vibarua.

Kwa faida hiyo iliyotangazwa inakadiriwa kuwa wafanyakazi hao wanaofanya kazi na kulipwa kwa idadi ya saa wanazofanya kazi wapatao 56,000 waliopo ndani ya Marekani watapata wastani wa mgawanyo wa faida wa $9,000 (TZS19m) kwa kuzingatia kiasi cha faida kilichopatikana Marekani ya Kaskazini.

Rais wa Marekani, Donald Trump aliwahi kuzilaumu kampuni kubwa za magari za Marekani, Ford na Genera Motors kwa kuongeza uzalishaji nchini Mexico na kuelekeza upanuzi wa biashara kwenye ukanda wa Marekani ya kati huku wamarekani wengi wakikosa ajira nchini kwao.

Baada ya kuapishwa kwa rais Trump, Ford ilitangaza kusitisha mpango wa kujenga karakana mpya nchini Mexico iliyotakiwa kugharimu $1.6bn na pia ikaokoa kiasi cha $500m kwa kuhamishia uzalishaji wa magari kwenye karakana iliyopo Flat Rock nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *