Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, DJ Khaled amepewa tuzo na RIAA (Recording Industry Association of America) baada ya single yake ya ‘For Free’ kufikisha mauzo ya Platinum.

DJ Khaled kupitia kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kuwa collabo yake na rapa Drake “For Free” imefikisha rekodi ya Platinum na kupewa tuzo ya RIAA.

Single hiyo, ilikuwa ya kwanza kuachiwa ndani ya albam yake ya tisa inayoitwa Major Key, ilifanya vizuri kwenye chart za Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya 13.

Hii sio mara ya kwanza kwa DJ Khaled kufikisha rekodi zake Platinum; single zake nyingine kama “I’m So Hood,” “I’m On One,” “All I Do Is Win,” “We Takin Over” na “I Wish You Would” zote hizi zilifanikiwa kupewa tuzo hiyo.

Pia DJ Khaled alishika nafasi ya kwanza kwenye chart ya Billboard upande wa albam bora za Hip Hop & R&B.

Dj Khaled ni mwanamuziki anayeongoza nchini Marekani kwa kushirikisha wasanii wengi ndani ya nyimbo moja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *