Kampuni ya EATV leo imeanza kutoa fomu kwa wasanii kwa ajili ya kushiriki katika tuzo za ‘EATV Awards’ zilizozinduliwa mapema mwezi Agosti mwaka huu ambapo zitakuwa zinashirikisha wasanii kutokaka ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkuu wa Masoko wa EATV, Roy Mbowe amesema leo wameanza kutoa fomu kawa ajili ya kushiriki kwenye tuzo hizo na mwisho wa kuchukua fomu na kuzirudisha ni Oktoba 22 saa 11 jioni.

Mbowe amesema fomu hizo zinaweza kujazwa na msanii mwenyewe au meneja wake, lakini pia lazima kuwepo na mashahidi watakaojaza pia. Wasanii watatakiwa kuzirudisha fomu hizi pamoja na kazi zao.

Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.

Vipengele hivyo ni:

 1. Mwanamuziki bora wa kiume
  2. Mwanamuziki bora wa kike
  3. Mwanamuziki bora chipukizi
  4. Kundi bora la muziki
  5. Video bora ya muziki
  6. Wimbo bora wa mwaka
  7. Muigizaji bora wa kiume
  8. Muigizaji bora wa kike
  9. Filamu bora ya mwaka
  10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.

Tuzo hizo zitatolewa December 10 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *