Bendi ya Muziki wa Dansi nchini, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wanatarajia kufanya onesho katika Ukumbi wa Hisaje Park, Boko jijini Dar es Salaam Agosti 12 mwaka huu.

Rais wa bendi hiyo, Nyosh Eld Saadat amesema kuwa usiku huo utakuwa wa aina yake kutokana na kuwepo kwa burudani tele siku hiyo hivyo amewaomba wapenzi na mashabiki wao wajitoekeze katika onesho hilo kwani burudani zitakuwa mwanzo mwisho.

nyoshi

Nyoshi Eld Saadat amesema kwamba watatambulisha staili mpya na sebene la aina mpya, kwa hiyo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia makamuzi ambayo hayajawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa bendi hilo.

Vile vile katika onesho hilo FM Academia watashirikiana na Yamoto Band usiku huo ambapo watapiga nyimbo zao zote kali huku wakizindua nyimbo zao mbili, Suu na Mijudo kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi huo wa Hisaje Park uliopo Boko jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *