Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwaka huu utakuwa ni wa mwisho kwake kutoa albam na kwamba atakuwa anaachia single ili aweze kuwapatia mashabiki zake nyimbo  nyingi mara kwa mara.

Flora amesema kuwa  hayo ndiyo mpango wake kwa miaka ijayo huku akitaka mashabiki wanamuona kuwa amekuwa kimya kwa muda mrefu kutambua kuwa muziki wa Injili upo tofauti na muziki wa bongo fleva ndiyo maana inakuwa rahisi kwa wasanii wa bongo fleva kuachia nyimbo mara kwa mara.

Amesema nyimbo za Injili zinahitaji kuwa na muda wakutosha na kumuomba Mungu ili akupatie mashairi mazuri yenye ujumbe ukisema ukurupuke na kuachia nyimbo kila siku utajikuta unatoa albamu nyingi lakini hit song ni moja na nyimbo nyingine zinasindikiza.

Utaratibu wa albam umepotea kwa muda mrefu katika tasnia ya burudani nchini (Tofauti na muziki wa injili) kwa madai kuwa hazina soko.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *