Mwanamitindo maarufu nchini, Flaviana Matata ameushitaki mfuko wa pensheni wa PSPF mahakamani akitaka alipwe shilingi milioni 165 kutokana na kosa la kukiuka mkataba wao wa kikazi.

Flaviana na mwanasheria wake Edward Lisso wa Law Associates Advocates wameushitaki mfuko huo kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mwanamitindo huyo ameiomba mahakama hiyo iuamuru mfuko huo kumlipa kiasi cha milioni 100 ikiwa ni kama fidia kutokana na kupoteza muda na fedha nyingi.

Pia Flaviana amesema amekosa fursa nyingi za kibiashara na makampuni mengine wakati akifanya mawasiliano na mlalamikiwa na ugumu alioupata wakati akifuatilia suala hilo.

Flaviana Matata pia ameongeza kusema kuwa anakula hasara ya kiuchumi kwa vile picha zake zinaendelea kutumika kinyume na mkataba wake walioingia na mfuko huo hapo awali.

Shauri hilo lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Magreth Bankika na litatajwa tena Septemba 22 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *