Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa misimu mingine zaidi.

Firmino ameasaini mkataba huo ambao utamfanya aweze kulipwa kiasi cha paundi 180,000 kwa wiki ambapo ni zaidi ya shilingi milioni 410 za Kitanzania.

Mkataba huo mpya wa miaka mitano unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2023 baada ya kukubaliana na klabu hiyo.

Mchezaji huyo mpaka sasa ameshinda magoli 15 kwenye ligi kuu nchini Uingereza pamoja kuisaidia klabu yake kufika hatua ya Nusu fainali ya kombe la klabu Bingwa barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *