Mshambuaji wa Liverpool, Roberto Firmino amekamatwa na polisi kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa amelewa siku ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekamatwa baada ya gari lake kusimamishwa katikati mwa jiji la  Liverpool mapema siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo wa Brazil anatarajiwa kufikishwa mbele ya hakimu wa jiji la Liverpool ifikapo Januari 31 mwakani.

Mshambuliaji huyo atawasilishwa mahakamani siku ambayo timu yake itacheza dhidi ya ya Chelsea katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ilimsajili mchambuliaji huyo kutoka Hoffenheim kwa kandarasi ya miaka mitano iliogharimu kitita cha pauni milioni 29 mwezi Juni.

Alicheza katika ushindi wa wiki iliopita dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park.

Liverpool imesema kuwa haitazungumzia swala hilo hadi pale hatua hiyo ya kisheria itakapokamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *