Filamu kuhusu shambulizi la kigaidi la Alshabaab nchini Kenya ambapo watu 28 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera mwaka 2014 imeshinda tuzo la Oscars kitengo cha wanafunzi.

Filamu hiyo inayoeleza hadithi ya Kenya, kuhusu Wakenya na inashirikisha waigizaji wa Kenya, inasimulia shambulio hilo la mwaka 2014 kaskazini mwa Kenya, ambapo maudhui ya uadui wa kidini kati ya wakristo na waislamu yanaangaziwa.

Tuzo hiyo itatolewa tarehe 12 Oktoba, katika ukumbi wa Samuel Goldwyn Theater, Beverly Hills, Los Angales Marekani.

Katika shambulizi hilo, Waiwslamu walikataa kujitenga na Wakristo walipoamriwa kufanya hivyo na magaidi wa Alshabaab kutoka Somalia.

Filamu hiyo iliyoundwa kwa ushirikiano wa wanafunzi wa Ujerumani na watengenezaji filamu wa Kenya inalenga kuwakumbuka mashujaa wa shambulizi hilo.

Kwa kipindi cha Zaidi ya miongo miwili, Kenya imekuwa ikishambuliwa na magaidi wa Alshabaab.

Mwaka 2015, wanafunzi zaidi ya 147 waliuwawa na Alshabaab katika chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *