Mugizaji wa Bongo movie,  Ahmed Bachu anatarajia kuingiza sokoni filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Fuko la Pesa’ ambayo imeshirikisha wasanii mbali mbali wanaofanya vizuri katika tasnia ya uigizaji hapa nchini.

Bacha amsema kuwa Fuko la pesa ni filamu ambayo itang’ara na kufungua njia kwa wasanii wake kwani kuanzia story hadi uigizaji imetendewa haki na washiriki, lakini production iliyotumika ni level za kimataifa kwani imefanywa na kampuni ya Proin muongozaji akiwa Lusubilo Mwanguku.

Baadhi ya Scene kwenye filamu ya Fuko la Pesa
Baadhi ya Scene kwenye filamu ya Fuko la Pesa

Filamu ya Fuko la Pesa imeandikwa na Zagamba Junior kuwashirikisha wasanii kama Riyama Ally, Dennis Louise na washiriki kutoka Tanzania Movie Talent (TMT) ni kazi ambayo Bachu anaamini inaenda kuonyesha umahiri wake katika uigizaji na uandaaji pia.

Bachu amejizolea umaarufu kwa kuwa kuandaa wasanii na kuwa ni moja kati ya mawakala wenye kuwa na wasanii wanzuri katika kazi za uigizaji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *