Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limetupilia mbali rufaa ya klabu ya Simba iliyowasilishwa kwenye shirikisho hilo kupinga Kagera Sugar kupewa pointi tatu.

Klabu ya Simba ilipeleka maombi ya kupinga Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuipa Kagera Sugar pointi tatu kufuatia kadi tatu za mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi

Katika barua ya FIFA iliyowasilishwa kwa Simba imesema kuwa maamuzi yanayofanywa na shirikisho la soka ndani ya nchi FIFA hawawezi kuyapangua.

Kutokana na rufaa hiyo kutupiliwa mbali, Yanga inaendelea kuwa bingwa kutoka na maamuzi hayo ambayo hayatabadili msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2016/17.

Kama Simba ingerejeshewa pointi hizo inamaana kuwa yenyewe ndiyo ingekuwa bingwa wa ligi hiyo kwa kuwa Yanga ilitwaa ikiwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa, licha ya timu zote hizo mbili kuwa na pointi sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *