Shirikisho la Soka Duniani Fifa limeongeza idadi ya timu kutoka 32 hadi 48 zitakazoshiriki kombe la duniani baada ya makubaliano yaliyofanyika mjini Zurich nchini Uswisi leo.

Mpango huo licha ya kupitishwa lakini utaanza kutekelezwa kuanzia michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 lakini fainali mbili zijazo timu zitakuwa kama zilivyokuwa 32.

Mswizi huyo, ambaye anasema ana uungwaji mkono mkubwa, anataka michuano hiyo iwe na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi.

Iwapo mpango huo utaidhinishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998.

Mapendekezo matano ambayo baraza kuu la Fifa lenye wanachama 37 limeangazia kama ifuatavyo.

  • Kombe la Dunia lenye timu 48 na makundi 16 ya timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya muondoano ya timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
  • Kombe la Dunia la timu 48, mechi moja ya muondoano wa kufuzu ambapo mshindi atajiunga na timu 16 nyingine (mechi 80 kwa jumla – 16 za muondoano wa kufuzu na 64 za michuano kamili).
  • Kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundini ndizo zinafuzu (makundi 76).
  • Kuwa na timu 40 na makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88).
  • Kusalia na Kombe la Dunia lilivyo sasa ambapo kuwa timu 32 (mechi 64).

Rais FIFA Gian Infantino amefanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo yenye mvuto mkubwa duniani.

Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *