Shirikisho la soka Duniani (FIFA)  limemfungia naodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye pia anaichezea FC Barcelona ya Hispania.

FIFA  wametangaza kumfungia mechi nne Lionel Messi kufuatia kosa alilolitenda March 24 wakati wa mchezo dhidi ya Chile.

messi

Messi amefungiwa kutokana na utovu wa nidhamu wa kumtolea lugha isiyo ya kiungwana refa wa mchezo huo.

Adhabu hiyo ya Lionel Messi inaambatana na faini ya pound 8100, hivyo kufuatia adhabu hiyo Lionel Messi sasa ameanza kuitumikia kwa kukosa game dhidi ya Bolivia leo iliyomalizika kwa Argentina kupoteza kwa goli 2-0.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *