Rais wa shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), Gianni Infantino ameunga mkono mapendekezo yaliyyotolewa na shirikisho la soka la bara la America Kusini (CONMEBOL) la kuongeza timu 16 kwenye fainali za Kombe la dunia 2022.

Akiongea kwenye mkutano wa CONMEBOL uliofanyika jijini Buenos Aires huko Argentina, ambapo alialikwa kama mgeni rasmi, Infantino amesema ombi hilo amelipokea lakini linahitaji kufanyiwa uchunguzi kama inawezekana kwa 2022.

FIFA tayari imeshapitisha mabadiliko kutoka timu 32 hadi 48 lakini ni kuanzia fainali za mwaka 2026 lakini CONMEBOL wao wanaona ni mbali zaidi badala yake mabadiliko hayo yaanze kwenye fainali za 2022.

Fainali hizo zitafanyika nchini Qatar ambapo Infantino amesema inabidi uchunguzi wa kina ufanyike endapo mazingira yataruhusu kuongeza timu hadi 48 na wao kama FIFA hawatakuwa na shida na hilo.

Wakati huo Qatar wamejipanga kujenga viwanja 8 ikiwa ni vinne pungufu kutoka kwenye idadi ya viwanja inayohitajika kwa timu 48. Endapo FIFA itaongeza timu basi mwenyeji wa mashindano anatakiwa kuwa na viwanja 12 au zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *