Shirikisho la Soka dunia (FIFA) limeanza kuchunguza uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United.

Fifa imeandika barua kwa klabu hiyo ya ligi kuu nchini Uingereza ikitaka maelezo zaidi kuhsu uhamisho huo.

Shirikisho hilo linataka kujua ni nani alyeshirikishwa katika uhamisho huo wa kitita cha pauni milioni 89.3 na ni fedha ngapi zilizolipwa.

Pogba anahudumia msimu wake wa pili katika uwanja wa Old Trafford, baada ya kuondoka katika klaabu hiyo na kuelekea Juventus kwa kitita cha pauni milioni 1.5 mwaka 2012.

Raia huyo wa Ufaransa mara ya kwanza alijiunga na United kutoka klabu ya Ufaransa ya Le Havre 2009 kwa hali ya utata.

Alirudi katika klabu hiyo msimu uliopita kwa kitita kilichovunja rekodi cha Euro milioni 105.

United pia ilikubali kuilipa Juventus Euro milioni 5 kwa malipo ya ziada pamoja na gharama nyengine iwapo Pogba atatia saini kandarasi mpya.

Wakati walipothibitisha uhamisho huo, Juventus ilisema kuwa uhamisho huo umeimarisha uchumi wa klabu hiyo na kufikia Euro milioni 72.6.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *